Karibu KKKT Kibamba DMP

Usharika wa Kibamba Umeendelea na jukumu la kushughulikia mahitaji ya msingi ya watu na kwa wakati huo huo kuendeleza kazi ya uinjilisti ikiwa ni jukumu la msingi la Kanisa kuwa mwalimu wa masikini, wasio na sauti na wanaodhulumiwa aidha katika kutekeleza majukumu hayo Usharika wa Kibamba unaye Mchungaji mmoja ambaye ndiye kiongozi mkuu wa shughuli zote za Usharika akisaidiana na Wainjilisti watatu, Mtunza fedha mmoja pamoja na Parish worker.

KKKT USHARIKA WA KIBAMBA DMP

Utangulizi, Dira,Ujumbe na Maadili

Utangulizi


Kanisa la kibamba lilianza kama mtaa mwaka 1975 ambapo mnamo Mwezi wa kwanza Mwaka 2003 ukawa Usharika mteule na mnamo tarehe 14.05.2003 ndipo ulipozinduliwa kuwa Usharika kamili. Usharika wa Kibamba upo umbali wa kilomita takribani thelathini (30) kutoka katikati ya jiji la Dar es salaam. Aidha mtaa wa kibamba uliaza na Wakristo kumi na tano (15) walioungana na Wakristo wa madhehebu mengine ya Anglikana na Roman Catholic wakisali kwa zamu katika Majengo ya Shule ya Msingi Kibamba ambapo Walutheri na wa Anglikana walisali pamoja na Roman Catholic wenyewe.

Mnamo mwaka 1976 baadhi wa wazee wa madhehebu haya matatu; Mzee C. A. Heri kama kiongozi, Marehemu Mzee W. J. Kihampa, Mzee H. Maeda, Mzee H. Mushendwa, Mzee Tumaini Paulo, Mama Nderingo Msaki na Marehemu Mzee Wandi walikutana na kuzungumza uwezekano wa kupata eneo la kuabudia. Pamoja na wazo lao hilo pia walimshirikisha mwenyekiti wa kijiji wakati huo Marehemu Mzee Juma Junguri.

Mawasiliano yalifanyika kati ya Mzee Heri na Mwenyekiti wa kijiji Mzee Junguri ambapo Mzee Junguri aliwezesha kupatikana kwa mwenye eneo hili Mzee Mwaipopo ndipo eneo likanunuliwa na walutheri kwa kushirikiana na wa anglikana kwa gharama ya shilingi mia saba (Tshs.700).

Mnamo mwaka 1978 madhehebu yote matatu waliacha kusali katika majengo ya shule ya msingi kibamba na kuhamia katika eneo lao ambapo waliaza kusalia chini ya mti wakiendelea kushirikiana mpaka walipo weza kujenga jingo la miti na kuendelea kesali humo kwa kupokezana kwa nyakati tofauti

Mnamo mwaka 1982 Roman Catholic waliweza kupata eneo lao nyuma ya Hospitali ya Kibamba ndipo walijenga jengo lao la kanisa na kuhamia huko. Hivyo basi jengo la miti liliendelea kutunzwa kwa kutumiwa na madhehebu ya lutherani na anglikana ambapo pia baada ya kipindi kidogo ndipo walutheri na wa anglikana waligawana eneo hili na walutheri wakaweza kujenga kanisa ambalo lilikamilika na kuhamiwa mwaka 1996 ambapo tunaabudia sasa na kuwaacha wa anglikana wakiendelea kuabudia kwenye kanisa la miti.

Usharika wa Kibamba umeendelea kukuwa hususani baada ya Wilaya ya Kinondoni kugawanywa hivyo Makao makuu ya Wilaya ya Ubungo kuhamia Kibamba pamoja na kuanzishwa kwa Hospitali ya Mloganzila ambayo ni tawi la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Kiuchumi na kijamii Usharika wa Kibamba unahudumia Mitaa Miwili ambayo ni Amani na Mperamumbi. Aidha Washarika wa Kibamba wamegawanyika katika matabaka tofauti tofauti wengi wao wakijishughulisha na shughuli binafsi na baadhi wachache wakiwa ni waajiriwa na kundi kubwa likiwa ni Vijana ambao hawana ajira rasmi.

DIRA (Vision)


Taarifa ya Maono hutoa mtazamo na mwelekeo wa baadaye wa Usharika ili kuwawezesha watumishi na Usharika kwa ujumla kuweza kutekeleza majukumu yao kwa madhumuni waliyoyakusudia kwa pamoja. Dira yetu kama Usharika ni: Kukubali na kubadili Jamii yetu na ujumbe na upendo wa Yesu Kristo
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kibamba lengo ni kuwapa watu nafasi ya kumfahamu Yesu Kristo ili kupata uzima wa milele. Kanisa limejengwa juu ya msingi wa Yesu Kristo, linaongozwa na Neno la Mungu kama linavyopatikana Agano la Kale na Agano Jipya (Biblia ya Kikristo), na limeimarishwa katika misingi ya sakramenti. KKKT linaongozwa na Mkuu wa Kanisa (Askofu Mkuu) pamoja na Maaskofu kutoka dayosisi zote, wakisaidiwa na wakuu wa Majimbo


UJUMBE (Mission)



Taarifa ya ujumbe inafupisha lengo la kuwepo kwa Usharika na jinsi matarajio ya washarika yatakavyofikiwa. Aidha ujumbe wa Usharika ni: Kuwafanya watu wote kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo na kuwageuza watu wote kuwa wafuasi kamili wa Yesu Kristo Pamoja na kuhakikisha Usharika wa Kibamba unakua endelevu na kupata mafanikio katika kutoa huduma ya Kichungaji kwa jamii, kuboresha Uinjilisti na huduma za misioni, uendelevu wa Kanisa pamoja na usimamizi bora wa rasilimali na miradi ya Usharika


MAADILI (Core Values)


Kazi ya Kanisa kwa ujumla inazingatiwa kwa maneno ya Yesu, 'Nenda ulimwenguni pote, na uhubiri injili kwa viumbe vyote.Mathayo 28: 18-20 Yesu akaja akawaambia, akisema, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, nendeni mkawafanye wanafunzi wa mataifa yote, na kuwabatiza kwa jina la Baba na wa Mwana na wa Roho Mtakatifu, na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi, na tazama, mimi nipo pamoja nayi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Maadili yetu yanategemea imani, katika kuamini Biblia na Ulutheri na upendo wetu kwa Mungu na jirani
  • Utukufu, huruma na haki (Dignity, compassion and justice)
  • Msamaha na upatanisho (Forgiveness and reconciliation)
  • Ujasiri na uwazi wa kubadilika (Courage and openness to change)
  • Uaminifu wa uumbaji wa viumbe na zawadi za Mungu (Faithful stewardship of Gods creation and gifts)
Prev Next
KKKT USHARIKA WA KIBAMBA DMP

RATIBA ZA IBADA

JUMAPILI

SAA 1:30 Hadi SAA 4:00 Asubuhi

Ibada hii itajumlisha na Ibada ya Watoto (Sunday School)

SAA: 4 :00 hadi Saa 7:00 Mchana

JUMA TANO

SAA 10:00 Hadi SAA 12:00 Jioni

Masomo ya Biblia (Bible Study)

IJUMAA

SAA 10:00 Hadi SAA 12:00 Jioni

Maombi na Maombezi.

JUMAMOSI

SAA 12:30 Hadi SAA 2:00 Asubuhi

Ibada za Jumuiya pamoja na Mazoezi ya Vikundi vya huduma.

KKKT USHARIKA WA KIBAMBA DMP

Huduma za Kiroho

SAKRAMENT NA NDOA

Huduma ya Chakula cha Bwana (Sakrament Takatifu) hutolewa, Ndoa Takatifu ufungishwa baada ya Mafundisho Karibu KKKT Kibamba

UBATIZO NA KIPAIMARA

Huduma za Ubatizo kwa Watoto na Watu Wazima sambamba na Mafundisho ya Kipaimara hutolewa Karibu KKKT Kibamba

MAOMBI NA MAOMBEZI

Huduma za Maombi na Maombezi hutolewa kwa kila muhitaji bila gharama, Kwa Jina La Yesu Kristo Karibu KKKT Kibamba

Wamtumainio Bwana ni Kama Mlima Sayuni

Loading...
http://besucherzählerkostenlos.com/